Umoja wa mataifa hii leo umeanza
kupeleka wanajeshi wake nchini Mali na kufikisha idadi ya wanajeshi
wanaoshika doria nchini humo na ambao watakuwa chini ya UN hadi, 6,000.
Idadi ya wanajeshi inatarajiwa kufika 12,640 mwisoni mwa Disemba.Jukumu lake la kwanza litakuwa kuhakikisha kuna usalama kabla ya uchaguzi wa urais kufanyika tarehe 28 mwezi huu.
Wapiganaji wa kiisilamu walianza kufanya harakati zao baada ya mapinduzi ya kijeshi yaliyomwondoa mamlakani rais wa taifa hilo huku wapiganaji wa kiisilamu wakitwa udhibiti wa eneo Kaskazini mwa nchi hiyo ikiwemo miji ya Gao, Kidal na Timbuktu ambako waliamuru kutumika kwa sheria kali za kiisilamu.
Ufaransa iliamua kuingilia mzozo huo, baada ya wapiganaji wa kisilamu kutishia kuvamia mji mkuu Bamako.
Tangu mwezi Januari, wanajeshi 4,000 wa Mali, wamechukua udhibiti wa sehemu kubwa ya miji mikubwa nchini humo, lakini wapiganaji kadhaa wamekuwa wakifanya mashambulizi ya kuvizia,
Jeshi la Umoja wa mataifa litajulikana kama Minusma na litahitaji kufanya kazi nzuri.
Harakati za jeshi la Ufaransa zimewafurahisha wengi kwa sababu wamekuwa wakitumia nguvu.
Lakini waasi wametoroka na wananchi wengi wa Mali wanahofia kuwa wanajeshi wa UN huenda wasitumie nguvu kama wanavyofanya wanajeshi wa Ufaransa.