Mwanafunzi wa chuo kikuu cha Dodoma
anayejulikana kwa jina la Boid Mwakitalima amefariki dunia baada
kugongwa na treni....Mwanafunzi huyo alikuwa mwaka wa tatu.
Taarifa zinaeleza kuwa,
mwanafunzi huyo alikuwa anatembea pembezoni mwa reli huku akiwa
ameweka "headphone" sikioni, hali iliyomfanya ashindwe kusikia ama
kuhisi chochote juu ya muungurumo wa treni hilo mpaka
lilipomsogelea karibu na kumsukuma pembeni ambapo aliangukia
chuma na kuaga dunia pale pale...
Makamu Mkuu wa Chuo kikuu cha Dodoma Prof.Idrisa Kikula akiwasili Collage ya Informatics
Mbele ni Mshauri wa wanafunzi ( dean of student) chuo kikuu cha dodoma, Nyuma ni mshauri wa wanafunzi, Pro.Anatory ( dean of students) collage ya informatics na Katikati ni Makamu mkuu wa chuo cha Dodoma...
------
Baada ya ajali hiyo,
mwanafunzi huyo alipelekwa chumba cha kuhifadhia maiti katika
hospitali ya Mkoa wa Domoma, "General hospital" ambapo leo hii
ameagwa na wanafunzi wenzake wa chuo kikuu cha Dodoma na
kusafirishwa kwenda nyumbani kwao Mbeya kwa mazishi..
Wanafunzi wakiuaga mwili wa marehemu kwa huzuni
Mkuu wa collage ya Informatics, Prof. Mvuma, akitoa
nasaha zake
Rais wa wanafunzi, collage ya informatics akitoa nasaha zake