Makamu
wa Kwanza wa Rais Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad, Mwenyekiti wa
Kamati ya Maridhiano Hassan Nassor Moyo (kushoto) na Mjumbe wa kamati
hiyo Ismail Jussa Ladhu, wakibadilishana mawazo kabla ya ufunguzi wa
kongamano la maridhiano lililofanyika hoteli ya bwawani.
June 3, 2013 By
MwanaKijijiInaonekana
kina Seif Sharrif na kina Karume hawataki hasa Zanzibar iwe dola huru
ikiwa na “mamlaka yake”. Kwa karibu miaka miwili sasa wameendelea
“kudai” Zanzibar “huru” huku wakipuuzia njia zote rahisi za kuweza
kufanya hivyo. Nimejaribu kwa kila namna kuwapa ushauri rahisi wa
kuiondoa Zanzibar kwenye Muungano na ikawa nchi huru na tukakutana UN,
SADC, na EA kama nchi huru majirani lakini ndugu zetu inaonekana
hawataki kuchagua njia hata moja. Badala yake wameendelea na nina
uhakika wataendelea kufanya mikutano mingine ya “kudai” Zanzibar huru.
Sasa najiuliza wanataka tuwasaidieje? Wanataka sisi tuwafukuze watoke
ili waseme tumewafukuza? Suala la Zanzibar kuwa na mamlaka yake kamili
liko mikononi mwa Wazanzibari peke yao.
1. Walipodai Bendera ya Zanzibar Tanzania bara hatukuulizwa; waliamua wakawa nayo
2. Walipotaka wimbo wa Taifa – Tanzania Bara hatukuulizwa; wakawa nao
3. Walipoamua kutangaza Zanzibar ni huru na kuainisha mipaka yake kupitia katiba yao walifanya hivyo bila Watu wa Bara kuulizwa.
Kuna ushahidi wa kutosha kabisa kuwa linapokuja suala la Zanzibar
kudai “uhuru” na alama za kuwa bado wao ni dola Zanzibar wana rekodi ya
kufanya hivyo bila kuomba kibali kutoka Dodoma au kwa watu wa bara. Sasa
kwanini kwenye “mamlaka kamili” ni kama vile “wanataka hawataki”? Kabla
sijaamua kuwapa pendekezo jingine naomba Wazanzibar wale asilimia 60
ambao wanaamini kutokana na wingi wao wanawakilisha msimamo wa
Wazanzibari wote wafanya mambo yafuatayo ili waharakishe kuitoa Zanzibar
kwenye “ukoloni” wa watu wa bara na kuirejesha kuwa ile nchi nzuri, ya
heri, ambapo watu wake wote walikuwa wanaishi kwa furaha na maridhiano
tangu enzi na enzi.
1. Chama cha CUF na wale wa CCM upande wa Zanzibar ambao wanaamini
Zanzibar inakaliwa na Bara kama koloni watangaze kutoutambua Muungano
huu kwa vile siyo halali.
2. Wakishafanya hilo la kwanza CUF na CCM Zanzibar wawaambie wabunge
wao walioko kwenye Bunge la Muungangano kujiuzulu mara moja ili warudi
Zanzibar
3. Wazanzibar wamuambie Makamu wa Rais wa Muungano Dr. Ghaib Bilali
pamoja na watumisho wengine wote walioko kwenye Utumishi wa Jamhuri ya
Muungano ambao ni Wazanzibari waachie nafasi zao zote ili kutekeleza
hilo la 1. Hii itauthibitishia ulimwengu na marafiki zao kuwa kweli wako
serious katika kutaka uhuru – huwezi kudai uhuru wakati huo huo
unatumikia serikali ile ile!
4. Ili kufanikisha hayo mambo matatu ya kwanza hapo juu na kuwa
yasionekane yamefanywa kiholela basi Baraza la Wawakilishi ambao lina
wasomi lifanye mambo mawili. Kwanza lilete hoja rasmi ya kuitaka
serikali kuandaa mswada wa Sheria ya kusimamia kura ya maoni
(referendum) ya jinsi Zanzibar itajitoa, ijitoe lini na vipi na kwa
mfumo gani. Na pili ni kuileta sheria hiyo ili ipitishwe na Wawakilishi.
5. Kwa vile inawezekana basi katika sheria hiyo ya No 4 hapo
itahitaji Bunge la Muungano liliridhie basi Baraza la Wawakilishi
lipitishe sheria hiyo na iridhiwe na Rais wa Zanzibar na hoja ya sheria
hiyo iletetwe na hao wabunge wa Zanzibar kwenye Bunge la Muungano (kabla
hawajatoka) ili Bunge la Muungano liipitishe na kuruhusu Zanzibar
kuanza mchakato wa kutoka kwenye Muungano na ili kwamba Bunge la
Muungano nalo liweke utaratibu wa kuhakikisha kuwa mali na haki za
Watanganyika Zanzibar haziangukii mikononi mwa Nchi ya Zanzibar!
6. Wazanzibari waharakishe kuweka tarehe ya kutaka kutoka kwenye
Muungano ili na sisi watu wa bara tuzidi kuwaombea ili matamanio yao na
njozi zao za kuirudisha Zanzibar ambayo inatawaliwa na Tanganyika
zitimie.
NB: Ikumbukwe kuwa watu wa bara hatutaki Muungano wa Mkataba.
Tunataka Zanzibar watoke bila ya kufuatiwa na kitu kingine chochote
zaidi ya mahusiano ya ujirani mwema wa nchi mbiili. Bila ya shaka
kutokana na historia inawezekana katika mfumo ujao kutakuwa na
makubalianao ya nchi mbili (bilateral agreements) ili kuhakikisha
Zanzibar inaendelea kuwa huru n.k nk
Sasa kama njia hizi zote hazichukuliwi; tuwasaidie vipi Wazanzibar hawa wanaotaka kutoka kufunga virago?
LET ZANZIBAR GO!!!