Wanamgambo wa al-Shabaab wamefanya mfululizo wa mashambulio ya
ukatili na uhalifu dhidi ya raia katika wiki za hivi karibuni --
utekaji, kukata vichwa na kupora Wasomali katika kupuuza kabisa sheria
za sharia ambazo kundi hilo linadai kuzitetea.
Tarehe 30 Mei, al-Shabaab waliagiza kuachiwa kwa wapiganaji wake
sita, waliotuhumiwa kwa kupora dola 6,000 kutoka katika duka la dawa
huko Baardheere na kuhukumiwa kukatwa mikono yao ya kuume.
"Nilikusanyika na kundi kubwa kutoka mjini kushuhudia adhabu ambayo
ingetolewa kwa wapiganaji sita wa al-Shabaab, kwani tulitarajia mikono
yao ya kuume kukatwa," alisema Yusra Nur Abdirahman, mwenye umri wa
miaka 28 na mkaazi wa Baardheere. "Cha ajabu, mwakilishi kutoka katika
kundi hili [aliyekuwa anahusika kutoa hukumu] Shekhe Aadan Nuh
alitangaza kwa kutumia kipaaza sauti kwamba wajahidina hao sita
wangepigwa viboko 39 kama adhabu ya kosa lao."
Alisema Nuh aliagiza dola 4,900 kurudishwa kwa mfamasia huyo, ambaye ni muungaji mkono al-Shabaab .
"Uamuzi huu wa aibu na wa kuchekesha ambao kwa hakika ulinishangaza
na niliuchukulia kama uliokusudiwa kudanganya na kupotosha watu na
kuhimiza wanachama wa kikundi hiki kupora mali binafsi na mali za
familia," Abdirahman aliiambia Sabahi.
Huu ni mfano tu wa hivi karibuni wa jinsi adhabu za al-Shabaab
zisivyo na msingi maalumu na za kinafiki, kwa kuwa wapiganaji walikutwa
na hatia ya makosa hawapaswi kuumia na adhabu zilizoagizwa, alisema,
akiongeza kwamba wapiganaji pia wameanzisha ulipizaji kisasi dhidi ya
raia wa Somalia, ikiwa ni pamoja na utekaji nyara au kuwakata vichwa
ndugu wa viongozi kutoka Gedo na Hiran.
Abdirahman aliviomba
vikosi vya serikali ya Somalia kukomesha vitendo vya kutisha vya al-Shabaab vya kuteka nyara, kuua, kutesa na kupiga.
Kukiuka sheria ya sharia
Huko Hiran, al-Shabaab imekuwa ikitoa amri ambazo hazina uhusiano na
sharia hivyo wanachama wake wanaweza kuepukana na ujambazi na uasherati,
alisema mkuu wa poilisi wa Hiran kanali Isaaq Ali Abdullahi.
Majaji wa Al-Shabaab hawaelewi kikamilifu falsafa ya sheria ya
kiislamu na kanuni za msingi za mfumo wa sheria wa haki na usiopendelea,
alisema. Uamuzi wao sio halali kwa sababu unachochewa kisiasa, una
kisasi na kuzingatia mfumo wa sheria wa kula njama, alisema.
Abdullahi aliishutumu al-Shabaab kwa kumkata kichwa mzee mwanaume na
kijana wa kiume tarehe 22 Mei huko Dudumo Qaris, kilometa 45 kaskazini
magharibi mwa Beledweyne. Wapiganaji pia waliiba dazeni za ngamia kutoka
vijijini, alisema.
"Muda umefika kuwasaka hao wasaliti kutoka al-Shabaab, ambao
wanahusiana na al-Qaeda, na kuwaondoa kutoka katika miji mbalimbali na
vijiji katika mkoa ili kukomesha uonevu, ukandamizaji, ubaguzi na
kudharau [raia]," Abdullahi aliiambia Sabahi.
"Tumefikia katika hali ambapo tunahitaji kutambua matamanio yetu, kwa
sababu hivi karibuni utambuzi wa uhuru utakuwa kwetu, ambao watu wetu
wanastahili kwa sababu ya kujitoa kwa kiasi kikubwa," alisema.
Ahmed Abdullahi Osman Inji, aliyekuwa kaimu mkuu wa usalama wa Hiran,
alisema waathirika wawili walikuwa mjomba wake mwenye miaka 90, Hussein
Aadan Toore, na mtoto wa kiume wa Toore. Wauaji waliwakata vichwa kwa
kutumia jambia kali na kuwaacha kuvuja damu hadi kifo.
Muda wowote utakaochukua, al-Shabaab siku moja watapigwa na viongozi
wao watatakiwa kwenda mbele ya mahakama ya kijeshi kujibu makosa ya
gizani, alisema Inji.
"Ulipuaji wa mabomu na ukataji vichwa hauwezi kuendelea," alisema
Inji. "Vikosi vya serikali vinachelewa kutekeleza operesheni zao za
kijeshi kuzuia njia [za al-Shabaab] zisizo na heshima zinazosababisha
maumivu na ugumu kuhusu watu wa Somalia, ambao walilazimishwa kumeza
machungu ya mateso na kunyimwa maisha ya kisasa."
Majaaliwa ya Wasomali 6 waliotekwa nyara bado hayajulikani
Mahali walipo wananchi hao sita bado haijulikani kwa karibia wiki
mbili baada ya wapiganaji washukiwa wa al-Shabaab waliwatorosha kutoka
katika Gedo tarehe 23 Mei.
Utekaji nyara ulifanyika kilometa 40 kati ya El Waq na Bu Sar,
alisema mkuu wa wilaya wa El Waq Sahal Malim Ali. Mamlaka baadaye
zilirejesha mabaki ya gari na pikipiki iliyoungua, ambayo wanamgambo
watuhumiwa walitumia katika operesheni hiyo kabla ya kuungua na
kuwaacha, alisema.
Ali alisema utawala wake bado unawasaka watekaji nyara.
Al-Shabaab hawajadaiwa kuhusika na utekaji nyara huo, lakini Ali
alisema njia ya mashambulizi imekuwa ni mbinu ya hivi karibuni ya
al-Shabaab, ambayo inatumia utoroshaji, ukataji vichwa, na utekaji nyara
wa wananchi na mali binafsi kukabiliana na woga wa wakaazi wa maeneo
yaliyo chini ya udhibiti wa serikali ya Somalia.
Kuyumba kutokana na kushindwa kwa jeshi,
al-Shabaab inajaribu kugawanya umaarufu kwa kuanzisha mapigano na
machafuko ya kikabila dhidi ya serikali, alisema, akiongeza kwamba watu
wa Somalia hawatakubali kutishiwa.
Hakuna sheria za sharia wala sheria za kimataifa zinazoruhusu utekaji
nyara, alisema Ali. Katika migogoro, sheria za ushirikishwaji wa muda
wa vita zitatumika kukamata maadui, lakini kuwashikilia raia kama mateka
ni kinyume cha sheria na ni mbinu zisizokubalika kwa kushurutisha,
alisema.