Mahakama ya rufaa nchini Mirsi
imeamuru rais wa zamani wa nchi hiyo, Hosni Mubarak hapaswi kuzuiliwa
tena kuhusiana na vifo vya waandamanaji waliofariki
wakati wa mapinduzi
yake.
Kesi dhidi ya Mubarak itasikilizwa tena huku akitaka uamuzi wa kufungwa maisha jela kubatilishwa.
Aidha Mubarak,aliyetawala Misri kwa miongo mitatu aling'olewa mamlakani katika mapinduzi ya kiraia mwaka 2011.
Amekuwa akizuiliwa tangu Aprili mwaka 2011 baada ya kuhusishwa na vifo vya mamia ya waandamanaji waliofanya maandamano ya amani wakimtaka aondoke mamlakani Januari kati ya tarehe 25-31.
Pia anakabiliwa na kesi ya ufisadi.
Mawakili wake walitaka mahakama kumwachilia Mubaraka kwani amezuiliwa kwa miaka miwili sasa na kulingana na sheria anapaswa kuachiliwa ikiwa kesi yake haijaamuliwa.