Karibu Pemba ni Blog yenye kukupa wingi wa habari na matukio yanayotokea kote duniani kwa lugha tofauti kiingereza kiswahili na hata kiarabu na lugha zoote ulimwenguni jiunge sasa kwa kupata habari moto moto
Friday, May 24, 2013
AIBU: MUME WA MTU ANASWA NA MWANAFUNZI WA KIDATO CHA PILI GESTI
INAUMA sana! Wakati wazazi wakihenyeka na wakati mwingine kujinyima ili mabinti zao waweze kupata elimu bora itakayowasaidia maishani mwao wapo wapuuzi wanaokatisha jitihada hizo.
Mwanaume mmoja aitwaye Taliki Juma mkazi wa Temeke – Wailesi jijini Dar es Salaam ameingia katika dimbwi la AIBU baada ya kunaswa akiwa na mwanafunzi wa kidato cha pili wakifanya mchezo mchafu.

Mbaya zaidi, bila haya wala soni, Taliki alimwingiza binti huyo (jina na shule anayosoma vinahifadhiwa kwa sababu za kimaadili) katika chumba anachoishi na mwanamke anayedaiwa ni mke wake ambaye alikuwa safarini.
Chanzo chetu cha habari kilipiga simu chumba cha habari na kueleza juu ya tabia ya Taliki ya kwenda na denti huyo chumbani kwake tena akiwa kwenye sare za shule.
Kikao cha dharura kiliitishwa haraka baada ya sosi
wetu kutoa maelekezo juu ya habari hiyo ambapo kwa muda huo na foleni za
jiji la Dar usafiri uliopendekezwa ukawa ni pikipiki.
Haraka timu ya waandishi wetu ilielekea eneo la tukio lakini kwa bahati mbaya walikwama.
Taarifa
iliyopatikana kutoka kwa mtoa habari wetu ni kwamba, muda mfupi kabla
timu haijaingia eneo la tukio, Taliki alifanikiwa kukwepa mtego baada ya
kumuondoa denti huyo.
Wikiendi iliyopita Mei 18, mwaka huu chanzo chetu kilekile kilipiga tena simu kwa mwandishi yuleyule na kueleza kuwa jamaa kwa mara nyingine amemwingiza yule denti chumbani kwake.
Timu A iliondoka na kwenda moja kwa moja hadi eneo
la tukio na kuliweka chini ya uangalizi huku timu B ikielekea katika
Kituo cha Polisi cha Wailesi na kuomba ushirikiano wao.
Timu ya maaskari wa kituo hicho wakiwa tayari kwa lolote, waliungana na waandishi wetu kwenda eneo la tukio.
Waandishi
wetu, maaskari na wazee wachache wa mtaani hapo walivamia katika chumba
hicho na kufanikiwa kumnasa laivu Taliki akiwa na denti huyo kama
walivyozaliwa akimfanyisha mambo ya kikubwa muda ambao alitakiwa kuwa
darasani.
Binti huyo ambaye alionekana kushtuka sana baada ya kukutwa chumbani hapo, alieleza kuwa amekuwa katika uhusiano na Taliki kwa muda mrefu baada ya kumrubuni kwa fedha na zawadi mbalimbali.
“Ni kweli huyu hapa ni mpenzi wangu, huwa ananipa pesa.
Nyumbani kwetu ni Mwananyamala na nimetoka nyumbani nikienda tuisheni
lakini Taliki aliniambia nije kwake.
“Naombeni mnisamehe jamani. Mama
akijua atanipiga sana. Nisameheni tafadhali na ninaahidi mbele yenu
kuwa nitaachana kabisa na huyu mbaba (Taliki),” alisema denti huyo.
Denti huyo alitoa namba ya simu ya mama yake
mzazi ambapo alipigiwa na kufika eneo la tukio na kujionea jinsi mtoto
wake anavyoharibiwa wakati yeye akiwa kwenye juhudi za kumtengenezea
maisha.
Mama wa binti huyo, hakuamini alichokiona na alijikuta akimwaga machozi muda wote, watu wazima wakapata kazi ya kumtuliza.
UPUUZI WA TALIKI
“Ni kweli nakubali huyu ni mpenzi wangu na nipo naye muda mrefu ila naombeni sana mnisamehe, kwa kweli ni shetani tu alinipitia (Mh! Huyu shetani anasingiziwa mengi sana).
“Ni kweli nakubali huyu ni mpenzi wangu na nipo naye muda mrefu ila naombeni sana mnisamehe, kwa kweli ni shetani tu alinipitia (Mh! Huyu shetani anasingiziwa mengi sana).
“Ndugu zangu
wakijua hili jambo watanitenga, naombeni muwe na roho ya huruma
(utadhani na yeye ana huruma), maisha yangu yataharibika (sijui alikuwa
anamtengenezea yule binti wa watu maisha?).”
Utetezi wake
haukusaidia na badala yake alifikishwa katika Kituo cha Polisi Wailesi
na kufunguliwa mashitaka katika Jalada namba WS/RB/585/2013 – KUFANYA
MAPENZI NA MWANAFUNZI.
Thursday, May 23, 2013
ASKARI ALIYENASWA NA MAGUNIA 18 YA BANGI HUKO HIMO AWATOROKA POLISI
ASKARI
Polisi Koplo Edward, anayedaiwa kusafirisha dawa za kulevya (bangi)
gunia 18 huko Himo, Kilimanjaro tarehe 18, Mei 2013, ametoroka chini ya
ulinzi wa askari polisi saba na kutokomea kusikojulikana.
Mtuhumiwa huyo alikuwa dereva wa gari aina ya Toyota Landcruiser namba PT. 2025 la Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) Mkoa wa Arusha.
Mtuhumiwa huyo alikuwa dereva wa gari aina ya Toyota Landcruiser namba PT. 2025 la Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) Mkoa wa Arusha.
Kamanda wa Polisi
Mkoa wa Arusha, Liberatus Sabas alisema askari huyo akiwa chini ya
ulinzi wa askari polisi saba, walikwenda nyumbani kwake kwa ajili ya
ukaguzi, na walipofika nyumbani kwa mtuhumiwa, walimwamini
na kumwacha kuingia ndani peke yake nao waliingia ndani ili kuendelea
na upekuzi, na ndipo mtuhumiwa alipofungua mlango wa nyuma ya nyumba
yake na kukimbia bila ya wao kufanikiwa kumkamata
Alisema
polisi imemkamata Inspekta wa Polisi Izaack Manoni aliyekuwa anasimamia
upekuzi huo: “Inspekta Manoni yupo chini ya ulinzi na hatua za kinidhamu
dhidi yake zitachukuliwa,” alisema ACP Sabas na kuongeza:
Alisema tayari mtuhumiwa mwenzake ambaye ni askari polisi mwenye namba G. 2434 PC George, amesomewa mashitaka yake jana.

Mbali na mtuhumiwa huyo, watuhumiwa wengine waliokamatwa na magunia 30 ya bangi wilayani Arumeru nao wamepandishwa kizimbani kusomewa mashitaka yao.
HALI BADO NI MBAYA MTWARA....WANAFUNZI WAWILI WAMETANDIKWA RISASI, MMOJA AMEFARIKI HAPOHAPO
Mwandishi wetu aliyepo Mtwara ametueleza kuwa hivi sasa baadhi ya wananchi wa eneo la magomeni mkoani mtwara wamekimbilia katika Hospitali ya Mkoa wa Mtwara Lugula wakihofia usalama wao kutokana na vurugu za kuchomwa kwa nyumba zao pamoja na vibanda vya biashara zilizotokea leo asubuhi katika eneo hilo..
Maduka maeneo ya Magomeni yamechomwa moto ikiwamo pia mali za Askari
magereza . Mwanafunzi wa CHUNO amefikishwa hospitali Ligula na majeraha ya risasi mguuni.
Mwanamke mwingine anayekadiriwa kuwa na miaka 25 mjamzito ameuawa kwa kupigwa risasi maiti ipo Ligula.





Kwa sasa ( jioni hii) inaelezwa kuwa katika baadhi ya mitaa hali imetulia na ni idadi ndogo ya wananchi ndiyo inayoonekana wakitembea mitaani isipokua eneo la magomeni ambako mbomu yanaendelea kusikika huku huduma za kijamii katika mji huo zikiwa zimesimama zikiwemo usafiri, huduma za kibenki na shule
PICHA ZA SHEHA WA TOMONDO- ZANZIBAR ALIYEMWAGIWA TINDIKALI JANA USIKU
Sheha
Mohammed Omary Said aliyemwagiwa tindikali na mtu asiyejulikana akiwa
katika hospitali ya Mnazi Mmoja Unguja akipatiwa matibabu, Sheikh
Mohammed amepata maumivu makali sehemu za kifuwa na jicho kuumia
Kamanda
wa polisi wa Mkoa wa Mjini Magharibi,Mukhadam Khamis,amesema chombo
kilichotumika kumwagia tindikali Sheha huyo kilipatikana eneo la tukio
na kwamba polisi imekichukua kwa kukichunguza kitaalam ili kugundua
aliyekuwa akikitumia kwa kuangalia alama za vidole.
Sheha huyo alimwagiwa tindikali jana usiku wakati alipotoka nje ya nyumba yake kuchota maji na ndipo mhalifu huyo alipomwagia tindikali na kwamba hakuweza kumtambua.
Sheha huyo alimwagiwa tindikali jana usiku wakati alipotoka nje ya nyumba yake kuchota maji na ndipo mhalifu huyo alipomwagia tindikali na kwamba hakuweza kumtambua.
Sheha
Mohammed Kidevu akiwa katika wodi ya Hospitali kuu ya Rufaa Mnazi Mmoja
akipata matibabu ya majaraha ya kitu kinachosadikiwa kwa Tindi
Kali,akipata matibabu hayo katika hospitali hiyo.
Wednesday, May 22, 2013
NYUMBA YA MWANDISHI WA HABARI WA TBC YACHOMWA MOTO HUKU MABOMU YAKIRINDIMA HUKO MTWARA
Hali imezidi kuwa mbaya katika Mji wa Mtwara na hivi punde watu wanaendelea kufanya uharibifu katika maeneo mbalimbali ya mji huo.
Jengo moja ambalo linadaiwa kumilikuwa na CCM limechomwa moto katika eneo la Majengo na daraja linalounganisha Lindi na Mtwara limevunjwa.
Mbali na hayo pia nyumba ya mwandishi wa habari wa Shirika la Utangazaji la Tanzania (TBC)imechomwa moto.
Katika Mji wa Mtwara milio ya mabomu na risasi ndio inayosikika kila kona. Jeshi la Polisi linajaribu kuwadhibiti vijana na watu wengine ambao wanafanya vurugu hizo.
MWANAFUNZI WA CHUO KIKUU CHA DODOMA AFARIKI DUNIA BAADA YA KUGONGWA NA TRENI
Mwanafunzi wa chuo kikuu cha Dodoma
anayejulikana kwa jina la Boid Mwakitalima amefariki dunia baada
kugongwa na treni....Mwanafunzi huyo alikuwa mwaka wa tatu.
Taarifa zinaeleza kuwa, mwanafunzi huyo alikuwa anatembea pembezoni mwa reli huku akiwa ameweka "headphone" sikioni, hali iliyomfanya ashindwe kusikia ama kuhisi chochote juu ya muungurumo wa treni hilo mpaka lilipomsogelea karibu na kumsukuma pembeni ambapo aliangukia chuma na kuaga dunia pale pale...
Makamu Mkuu wa Chuo kikuu cha Dodoma Prof.Idrisa Kikula akiwasili Collage ya Informatics
Mbele ni Mshauri wa wanafunzi ( dean of student) chuo kikuu cha dodoma, Nyuma ni mshauri wa wanafunzi, Pro.Anatory ( dean of students) collage ya informatics na Katikati ni Makamu mkuu wa chuo cha Dodoma...
------
Baada ya ajali hiyo,
mwanafunzi huyo alipelekwa chumba cha kuhifadhia maiti katika
hospitali ya Mkoa wa Domoma, "General hospital" ambapo leo hii
ameagwa na wanafunzi wenzake wa chuo kikuu cha Dodoma na
kusafirishwa kwenda nyumbani kwao Mbeya kwa mazishi..
Wanafunzi wakiuaga mwili wa marehemu kwa huzuni
Mkuu wa collage ya Informatics, Prof. Mvuma, akitoa
nasaha zake
Rais wa wanafunzi, collage ya informatics akitoa nasaha zake
Subscribe to:
Posts (Atom)


















