Thursday, May 23, 2013

ASKARI ALIYENASWA NA MAGUNIA 18 YA BANGI HUKO HIMO AWATOROKA POLISI

ASKARI Polisi Koplo Edward, anayedaiwa kusafirisha dawa za kulevya (bangi) gunia 18 huko Himo, Kilimanjaro tarehe 18, Mei 2013, ametoroka chini ya ulinzi wa askari polisi saba na kutokomea kusikojulikana.

Mtuhumiwa huyo alikuwa dereva wa gari aina ya Toyota Landcruiser namba PT. 2025 la Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) Mkoa wa Arusha. 
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Liberatus Sabas alisema askari huyo akiwa chini ya ulinzi wa askari polisi saba, walikwenda nyumbani kwake kwa ajili ya ukaguzi, na walipofika nyumbani kwa  mtuhumiwa, walimwamini na kumwacha kuingia ndani peke yake nao waliingia ndani ili kuendelea na upekuzi, na ndipo mtuhumiwa alipofungua mlango wa nyuma ya nyumba yake na kukimbia bila ya wao kufanikiwa kumkamata
 

Alisema polisi imemkamata Inspekta wa Polisi Izaack Manoni aliyekuwa anasimamia upekuzi huo: “Inspekta Manoni yupo chini ya ulinzi na hatua za kinidhamu dhidi yake zitachukuliwa,” alisema ACP Sabas na kuongeza:  
“Mtuhumiwa Edward, anayetafutwa kwa sasa alishafukuzwa kazi, akipatikana atafikishwa mahakama ya kiraia kusomewa mashitaka ya kufanya biashara ya dawa za kulevya,” alisema.

Alisema tayari mtuhumiwa mwenzake ambaye ni askari polisi mwenye namba G. 2434 PC George, amesomewa mashitaka yake jana.


Mbali na mtuhumiwa huyo, watuhumiwa wengine waliokamatwa na magunia 30 ya bangi wilayani Arumeru nao wamepandishwa kizimbani kusomewa mashitaka yao.

HALI BADO NI MBAYA MTWARA....WANAFUNZI WAWILI WAMETANDIKWA RISASI, MMOJA AMEFARIKI HAPOHAPO

Mwandishi wetu aliyepo Mtwara ametueleza kuwa hivi sasa baadhi ya wananchi wa eneo la magomeni mkoani mtwara wamekimbilia katika Hospitali ya Mkoa wa Mtwara Lugula wakihofia usalama wao kutokana na vurugu za kuchomwa kwa nyumba zao pamoja na vibanda vya biashara zilizotokea leo asubuhi katika eneo hilo..

Maduka maeneo ya Magomeni yamechomwa moto ikiwamo pia mali za Askari magereza . Mwanafunzi wa CHUNO amefikishwa hospitali Ligula na majeraha ya risasi mguuni.  
Mwanamke mwingine anayekadiriwa kuwa na miaka 25 mjamzito ameuawa kwa kupigwa risasi maiti ipo Ligula.




Kwa sasa ( jioni  hii) inaelezwa kuwa katika baadhi ya mitaa hali imetulia na ni idadi ndogo ya wananchi ndiyo inayoonekana wakitembea mitaani isipokua eneo la magomeni ambako mbomu yanaendelea kusikika huku huduma za kijamii katika mji huo zikiwa zimesimama zikiwemo usafiri, huduma za kibenki na shule

PICHA ZA SHEHA WA TOMONDO- ZANZIBAR ALIYEMWAGIWA TINDIKALI JANA USIKU

\
Sheha Mohammed Omary Said aliyemwagiwa tindikali na mtu asiyejulikana akiwa katika hospitali ya Mnazi Mmoja Unguja akipatiwa matibabu, Sheikh Mohammed amepata maumivu makali sehemu za kifuwa na jicho kuumia

Kamanda wa polisi wa Mkoa wa Mjini Magharibi,Mukhadam Khamis,amesema chombo kilichotumika kumwagia tindikali Sheha huyo kilipatikana eneo la tukio na kwamba polisi imekichukua kwa kukichunguza kitaalam ili kugundua aliyekuwa akikitumia kwa kuangalia alama za vidole.

Sheha huyo alimwagiwa tindikali jana usiku wakati alipotoka nje ya nyumba yake kuchota maji na ndipo mhalifu huyo alipomwagia tindikali na kwamba hakuweza kumtambua.

Sheha Mohammed Kidevu akiwa katika wodi ya Hospitali kuu ya Rufaa Mnazi Mmoja akipata matibabu ya majaraha ya kitu kinachosadikiwa kwa Tindi Kali,akipata matibabu hayo katika hospitali hiyo.

Wednesday, May 22, 2013

NYUMBA YA MWANDISHI WA HABARI WA TBC YACHOMWA MOTO HUKU MABOMU YAKIRINDIMA HUKO MTWARA


Hali imezidi kuwa mbaya katika Mji wa Mtwara na hivi punde watu wanaendelea kufanya uharibifu katika maeneo mbalimbali ya mji huo.

Jengo moja ambalo linadaiwa kumilikuwa na CCM limechomwa moto katika eneo la Majengo na daraja linalounganisha Lindi na Mtwara limevunjwa.


Mbali na hayo pia nyumba ya mwandishi wa habari wa Shirika la Utangazaji la Tanzania (TBC)imechomwa moto.

Katika Mji wa Mtwara milio ya mabomu na risasi ndio inayosikika kila kona. Jeshi la Polisi linajaribu kuwadhibiti vijana  na watu wengine ambao wanafanya vurugu hizo.

MWANAFUNZI WA CHUO KIKUU CHA DODOMA AFARIKI DUNIA BAADA YA KUGONGWA NA TRENI



Mwanafunzi  wa chuo kikuu cha Dodoma  anayejulikana  kwa jina  la Boid Mwakitalima  amefariki dunia  baada  kugongwa na treni....Mwanafunzi huyo  alikuwa  mwaka  wa  tatu.

Taarifa zinaeleza  kuwa, mwanafunzi  huyo  alikuwa   anatembea pembezoni  mwa  reli huku  akiwa ameweka  "headphone"  sikioni, hali  iliyomfanya  ashindwe  kusikia ama  kuhisi  chochote  juu  ya  muungurumo  wa  treni  hilo  mpaka  lilipomsogelea  karibu  na  kumsukuma  pembeni  ambapo  aliangukia  chuma  na  kuaga  dunia  pale  pale...
 Makamu Mkuu wa Chuo kikuu  cha Dodoma Prof.Idrisa Kikula  akiwasili Collage ya Informatics

 Mbele  ni Mshauri wa wanafunzi ( dean of student) chuo kikuu cha dodoma, Nyuma ni mshauri wa wanafunzi, Pro.Anatory  ( dean of students)  collage ya informatics na Katikati ni Makamu mkuu wa chuo cha Dodoma...
------ Baada  ya  ajali  hiyo, mwanafunzi  huyo  alipelekwa  chumba  cha kuhifadhia  maiti  katika  hospitali  ya  Mkoa  wa Domoma, "General hospital" ambapo  leo  hii  ameagwa  na wanafunzi wenzake  wa  chuo  kikuu  cha Dodoma  na  kusafirishwa  kwenda  nyumbani  kwao Mbeya kwa  mazishi..
 Wanafunzi wakiuaga  mwili  wa  marehemu  kwa  huzuni
 Mkuu wa  collage ya Informatics, Prof. Mvuma,  akitoa  
nasaha  zake
 Rais  wa wanafunzi, collage ya informatics  akitoa  nasaha  zake

VURUGU ZA MTWARA ZASABABISHA BUNGE LIAHIRISHWE

Hivi ndivyo kunavyoendelea hadi sasa Mkoani Mtwara
Spika wa bunge , Anne Makinda ameahirisha Bunge kutokana na hali ya Mtwara na ameiagiza serikali kuwa kesho wawasilishe taarifa bungeni kuhusiana na hali hiyo.

Makinda ameitisha kamati ya uongozi ili kuona kama wanaweza kutuma kamati ya Bunge kesho kwenda huko.

MKENYA ANAYELIA BAADA YA OBAMA KUPANGA KUJA TANZANIA NA KUIKACHA KENYA



Rais wa Marekani Barack Obama na mkewe Michelle mwezi ujao atakuwa na ziara katika nchi tatu za Afrika zikiwemo Tanzania, Afrika Kusini na Senegal.
Ziara hiyo itaanza June 26 – July 3. Hata hivyo kitendo cha Obama kuiruka Kenya nchi anayotokea baba yake mzazi, kimewaumiza wakenya wengi hasa ukizingatia kuwa hajawahi kuitembelea nchi hiyo tangu aingie madarakani.