
Na Fidelis Butahe, Mwananchi
Dar es Salaam: Kwa mara ya kwanza Rais Jakaya Kikwete amemtolea uvivu
 Rais wa Rwanda, Paul Kagame kutokana na kitendo chake cha kumtolea 
lugha za matusi baada ya kumshauri kukaa meza moja na vikundi vya waasi 
wa nchi yake (FDLR), huku akimtaka kuacha kukuza mgogoro usiokuwepo.
Rais Kikwete alitoa ushauri huo kwa Rwanda takribani miezi miwili 
iliyopita wakati akizungumza katika kikao cha Mkutano wa Umoja wa Afrika
 (AU) uliofanyika mapema mwaka huu, mjini Addis Ababa, Ethiopia, ambao 
ulikuwa ukijadili suala la amani ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo 
(DRC) pamoja na Ukanda wa Maziwa Makuu.
Ushauri huo pia uliwagusa Rais Yoweri Museveni wa Uganda na Joseph 
Kabila (DRC), ambao aliwataka kufanya mazungumzo na waasi wanaopingana 
na Serikali zao. Akizungumza katika hotuba yake ya kila mwezi Rais 
Kikwete alisema: “Ushauri ule niliutoa kwa nia njema kabisa, kwani bado 
naamini kuwa kama jambo linaweza kumalizwa kwa njia ya mazungumzo njia 
hiyo ni vyema itumike,”
“Isitoshe, ushauri ule niliutoa pia kwa Serikali ya Congo , Serikali 
ya Uganda. Katika mkutano ule Rais Museveni wa Uganda aliunga mkono 
kauli yangu. Rais Kagame hakusema chochote pale mkutanoni. Baada ya 
kurudi nyumbani ndipo tukaanza kuyasikia maneno tuliyoyasikia na 
tunayoendelea kuyasikia.”
Alisisitiza, “Kwa upande wangu sijasema lolote kuhusu Rwanda pamoja 
na maneno mengi ya matusi na kejeli yanayotoka kwenye vinywa vya 
viongozi wa Rwanda dhidi yangu. Siyo kwamba siambiwi yanayosemwa au 
sijui kusema au sina la kusema, la hasha, sijafanya hivyo kwa sababu 
sioni faida yake.”
Rais Kagame alitoa lugha zisizostahili dhidi ya Rais Kikwete katika 
sherehe ya kuhitimu mafunzo ya kijeshi ya maofisa 45 wa jeshi lake Julai
 mwaka huu, ambapo alisema ushauri wa kufanya mazungumzo na waasi wa 
FDLR ni ujinga na haupo katika historia ya Wanyarwanda.
“Nilinyamaza kimya kwa sababu sikupenda kusikiliza ushauri kuhusu 
FDLR, kwa sababu nafikiri ni upuuzi ulioambatana na ujinga. Hatuwezi 
kuacha maisha yetu kama Wanyarwanda tunavyoishi sasa. Ushauri wa Kikwete
 ni sawa na kucheza na makaburi ya watu wengi ambao ni ndugu zetu,” 
alisema Kagame.
Katika hotuba ya jana Rais Kikwete alisema uhusiano wa Tanzania na 
Rwanda unapitia katika wakati mgumu na mtikisiko, baada ya yeye kutoa 
ushauri kwa Serikali ya Rwanda kuzungumza na mahasimu wao na kwamba hilo
 linadhihirika katika kauli zinazotolewa na viongozi wa Rwanda.
“Napenda kuwahakikishia Watanzania wenzangu na ndugu zetu wa Rwanda 
kuwa mimi, Serikali ninayoiongoza na wananchi wa Tanzania ,tunapenda 
kuwa na uhusiano mzuri na ushirikiano wa karibu na Rwanda kama ilivyo 
kwa nchi zote jirani” alisema Rais Kikwete.
Alisema nchi hizo ni jirani na kila moja inamuhitaji mwenzake, hivyo lazima ziwe na uhusiano mwema na ushirikiano mzuri.
“Nasisitiza kuwa mimi na Serikali ninayoiongoza tutakuwa wa mwisho 
kufanya kitendo au vitendo vibaya dhidi ya Rwanda au nchi yoyote jirani 
au yoyote duniani. Hatuna sababu ya kufanya hivyo, kwani ni mambo ambayo
 hayana tija wala masilahi kwetu” alisema.
Alisema nchi hizo mbili zimekuwa zikijihusisha na mambo ya kukuza na 
kujenga ujirani mwema, kusisitiza kwamba hiyo ni moja ya nguzo kuu ya 
Sera ya Mambo ya Nje ya Tanzania.
“Nawahakikishia ndugu zetu wa Rwanda kuwa kwa upande wetu hakuna 
kilichobadilika wala kupungua katika uhusiano na ushirikiano wetu,” 
alisema na kuongeza;
“Kwangu sioni kama kuna mgogoro wa aina yoyote. Busara inatuelekeza 
kuwa tusikuze mgogoro usiokuwepo ‘Two wrongs do not make a right’ 
(makosa mawili hayawezi kutengeneza usahihi). Tunashirikiana na 
kusaidiana kwa mambo mengi baina ya nchi zetu kitaifa na katika kanda 
yetu ya Afrika Mashariki na Nchi za Maziwa Makuu, katika Umoja wa Afrika
 na hata kimataifa.”
Alifafanua kuwa alitoa ushauri huo kwa kuzingatia mila na desturi za miaka mingi katika ukanda wa Afrika Mashariki.
“Tumekuwa tunakutana katika mikutano na vikao mbalimbali tunazungumza
 na kushauriana kwa uwazi juu ya njia za kushughulikia matatizo na 
masuala mbalimbali kila yanapotokea,” alisema Rais Kikwete.
Alisema wakati wote matatizo yanazozikabili nchi za Afrika viongozi 
wote huyachukulia kama mambo yanayowahusu na kupeana ushauri, jambo 
ambalo alisisitiza kuwa ni wajibu kwa viongozi.
“Iweje leo mtu kutoa ushauri ule ionekane jambo baya na la ajabu. 
Jambo la kushutumiwa na kutukanwa, siyo sawa hata kidogo, Ushauri si 
shuruti, ushauri si amri. Una hiyari ya kuukubali au kuukataa” alisema 
Rais Kikwete na kuongeza;
“Muungwana hujibu, “Siuafiki ushauri wako”. Hakuna haja ya kutukana 
wala kusema maneno yasiyostahili wala kusema yasiyokuwepo na ya uongo.”
Rais Kikwete alisema Serikali ya Tanzania haina ugomvi wala nia mbaya
 na Rwanda na inapenda kuendelea na uhusiano mzuri na nchi hiyo.
“Labda wenzetu wanalo lao jambo dhidi yetu ambalo sisi hatulijui. 
Sisi tunasikia mengi yanayozungumzwa na kudaiwa kupangwa kufanywa na 
Rwanda dhidi yangu na nchi yetu. Hatupendi kuyaamini moja kwa moja 
tunayoyasikia lakini hatuyapuuzi” alisema.
Ushauri wa Rais Kikwete kwa Rwanda pia uliungwa mkono na Rais wa 
Marekani, Barack Obama wakati wa ziara yake nchini Tanzania, alipoitaka 
nchi hiyo kumaliza mgogoro wake na waasi kwa njia ya mazungumzo.
Katika hotuba hiyo, Rais Kikwete alizungumzia jinsi nchi 
ilivyonufaika na ziara ya Rais wa Marekani, Barack Obama, Rais mstaafu 
wa nchi hiyo, George W. Bush, Waziri Mkuu wa Thailand, Yingluck 
Shinawatra.
Photo: Rais Kikwete amvaa Kagame, amshangaa kwa lugha za matusi na 
kejeli Na Fidelis Butahe, Mwananchi Dar es Salaam: Kwa mara ya kwanza 
Rais Jakaya Kikwete amemtolea uvivu Rais wa Rwanda, Paul Kagame kutokana
 na kitendo chake cha kumtolea lugha za matusi baada ya kumshauri kukaa 
meza moja na vikundi vya waasi wa nchi yake (FDLR), huku akimtaka kuacha
 kukuza mgogoro usiokuwepo. Rais Kikwete alitoa ushauri huo kwa Rwanda 
takribani miezi miwili iliyopita wakati akizungumza katika kikao cha 
Mkutano wa Umoja wa Afrika (AU) uliofanyika mapema mwaka huu, mjini 
Addis Ababa, Ethiopia, ambao ulikuwa ukijadili suala la amani ya Jamhuri
 ya Kidemokrasi ya Congo (DRC) pamoja na Ukanda wa Maziwa Makuu. Ushauri
 huo pia uliwagusa Rais Yoweri Museveni wa Uganda na Joseph Kabila 
(DRC), ambao aliwataka kufanya mazungumzo na waasi wanaopingana na 
Serikali zao. Akizungumza katika hotuba yake ya kila mwezi Rais Kikwete 
alisema: “Ushauri ule niliutoa kwa nia njema kabisa, kwani bado naamini 
kuwa kama jambo linaweza kumalizwa kwa njia ya mazungumzo njia hiyo ni 
vyema itumike,” “Isitoshe, ushauri ule niliutoa pia kwa Serikali ya 
Congo , Serikali ya Uganda. Katika mkutano ule Rais Museveni wa Uganda 
aliunga mkono kauli yangu. Rais Kagame hakusema chochote pale mkutanoni.
 Baada ya kurudi nyumbani ndipo tukaanza kuyasikia maneno tuliyoyasikia 
na tunayoendelea kuyasikia.” Alisisitiza, “Kwa upande wangu sijasema 
lolote kuhusu Rwanda pamoja na maneno mengi ya matusi na kejeli 
yanayotoka kwenye vinywa vya viongozi wa Rwanda dhidi yangu. Siyo kwamba
 siambiwi yanayosemwa au sijui kusema au sina la kusema, la hasha, 
sijafanya hivyo kwa sababu sioni faida yake.” Rais Kagame alitoa lugha 
zisizostahili dhidi ya Rais Kikwete katika sherehe ya kuhitimu mafunzo 
ya kijeshi ya maofisa 45 wa jeshi lake Julai mwaka huu, ambapo alisema 
ushauri wa kufanya mazungumzo na waasi wa FDLR ni ujinga na haupo katika
 historia ya Wanyarwanda. “Nilinyamaza kimya kwa sababu sikupenda 
kusikiliza ushauri kuhusu FDLR, kwa sababu nafikiri ni upuuzi 
ulioambatana na ujinga. Hatuwezi kuacha maisha yetu kama Wanyarwanda 
tunavyoishi sasa. Ushauri wa Kikwete ni sawa na kucheza na makaburi ya 
watu wengi ambao ni ndugu zetu,” alisema Kagame. Katika hotuba ya jana 
Rais Kikwete alisema uhusiano wa Tanzania na Rwanda unapitia katika 
wakati mgumu na mtikisiko, baada ya yeye kutoa ushauri kwa Serikali ya 
Rwanda kuzungumza na mahasimu wao na kwamba hilo linadhihirika katika 
kauli zinazotolewa na viongozi wa Rwanda. “Napenda kuwahakikishia 
Watanzania wenzangu na ndugu zetu wa Rwanda kuwa mimi, Serikali 
ninayoiongoza na wananchi wa Tanzania ,tunapenda kuwa na uhusiano mzuri 
na ushirikiano wa karibu na Rwanda kama ilivyo kwa nchi zote jirani” 
alisema Rais Kikwete. Alisema nchi hizo ni jirani na kila moja 
inamuhitaji mwenzake, hivyo lazima ziwe na uhusiano mwema na ushirikiano
 mzuri. “Nasisitiza kuwa mimi na Serikali ninayoiongoza tutakuwa wa 
mwisho kufanya kitendo au vitendo vibaya dhidi ya Rwanda au nchi yoyote 
jirani au yoyote duniani. Hatuna sababu ya kufanya hivyo, kwani ni mambo
 ambayo hayana tija wala masilahi kwetu” alisema. Alisema nchi hizo 
mbili zimekuwa zikijihusisha na mambo ya kukuza na kujenga ujirani 
mwema, kusisitiza kwamba hiyo ni moja ya nguzo kuu ya Sera ya Mambo ya 
Nje ya Tanzania. “Nawahakikishia ndugu zetu wa Rwanda kuwa kwa upande 
wetu hakuna kilichobadilika wala kupungua katika uhusiano na ushirikiano
 wetu,” alisema na kuongeza; “Kwangu sioni kama kuna mgogoro wa aina 
yoyote. Busara inatuelekeza kuwa tusikuze mgogoro usiokuwepo ‘Two wrongs
 do not make a right’ (makosa mawili hayawezi kutengeneza usahihi). 
Tunashirikiana na kusaidiana kwa mambo mengi baina ya nchi zetu kitaifa 
na katika kanda yetu ya Afrika Mashariki na Nchi za Maziwa Makuu, katika
 Umoja wa Afrika na hata kimataifa.” Alifafanua kuwa alitoa ushauri huo 
kwa kuzingatia mila na desturi za miaka mingi katika ukanda wa Afrika 
Mashariki. “Tumekuwa tunakutana katika mikutano na vikao mbalimbali 
tunazungumza na kushauriana kwa uwazi juu ya njia za kushughulikia 
matatizo na masuala mbalimbali kila yanapotokea,” alisema Rais Kikwete. 
Alisema wakati wote matatizo yanazozikabili nchi za Afrika viongozi wote
 huyachukulia kama mambo yanayowahusu na kupeana ushauri, jambo ambalo 
alisisitiza kuwa ni wajibu kwa viongozi. “Iweje leo mtu kutoa ushauri 
ule ionekane jambo baya na la ajabu. Jambo la kushutumiwa na kutukanwa, 
siyo sawa hata kidogo, Ushauri si shuruti, ushauri si amri. Una hiyari 
ya kuukubali au kuukataa” alisema Rais Kikwete na kuongeza; “Muungwana 
hujibu, “Siuafiki ushauri wako”. Hakuna haja ya kutukana wala kusema 
maneno yasiyostahili wala kusema yasiyokuwepo na ya uongo.” Rais Kikwete
 alisema Serikali ya Tanzania haina ugomvi wala nia mbaya na Rwanda na 
inapenda kuendelea na uhusiano mzuri na nchi hiyo. “Labda wenzetu wanalo
 lao jambo dhidi yetu ambalo sisi hatulijui. Sisi tunasikia mengi 
yanayozungumzwa na kudaiwa kupangwa kufanywa na Rwanda dhidi yangu na 
nchi yetu. Hatupendi kuyaamini moja kwa moja tunayoyasikia lakini 
hatuyapuuzi” alisema. Ushauri wa Rais Kikwete kwa Rwanda pia uliungwa 
mkono na Rais wa Marekani, Barack Obama wakati wa ziara yake nchini 
Tanzania, alipoitaka nchi hiyo kumaliza mgogoro wake na waasi kwa njia 
ya mazungumzo. Katika hotuba hiyo, Rais Kikwete alizungumzia jinsi nchi 
ilivyonufaika na ziara ya Rais wa Marekani, Barack Obama, Rais mstaafu 
wa nchi hiyo, George W. Bush, Waziri Mkuu wa Thailand, Yingluck 
Shinawatra.